Thursday, 18 May 2017

Shairi Njoo

Shairi njoo, shairi njoo,
Mara nyingi kwangu mawazo yaja kwa Kiingereza, Kiswahili sasa nimeamua kujieleza.
Tangu nitoke skuli, Kiswahili niliweka kando,
Usidhani nikakidharau, La!
Mbali Kiingereza nikapenda.

Shairi njoo, Shairi njoo,
Utamu wa lugha umezidi, usifikiri Kiswahili sitamani,
Usidhani shairi siwezi tunga, usidhani la kusema siwezi pata.

Shairi njoo, shairi njoo,
Mapenzi, huzuni, dini, gani shairi nitaandika?
Mawazo ninayo, kalamu ninayo,
Lakini utajiri wa lugha kidogo umepungua, kamusi basi nitahitaji

Shairi njoo, shairi njoo,
Shairi ninayo, ngoja kidogo vitenzi nijikumbushe.
Methali pia niangalie, vitabu pia nisome.
Shairi laja, shairi laja,
Hivi punde!

No comments:

Post a Comment